phone: +255 718 561 149
e-mail: mitwecharitablefoundation@gmail.com

History


                                                   UTANGULIZI
Mitwe Charitable Foundation ni Taasisi ya Kujitolea ya Kitanzania isiyo ya Kiserikali iliyo Anzishwa rasmi mwaka 2012 nakupata usajili rasmi 13th, October ,2014  NO. 4977  chini ya Wizara ya Katiba na Sheria Kitengo cha RITA .Ikilenga kuwasaidia watu wenye mahitaji Maalum Tanzania na Africa kwa ujumla, kuwapatia msaada na mafunzo ya kiufundi(ELIMU).

                                 DIRA/NDOTO YA TAASISI
kuwa taasisi ya mfano inayowatafutia misaada mbalimbali Watoto wenye mahitaji maalumu na Mayatima hasa misaada inayofungamana na Elimu,Afya na yakijamii kwa ujumla.
     
                              UJUMBE WA M.C.F
Kuwakumbusha na kuwahamasisha watu wenye moyo na huruma kufanya kazi ya kujitolea na kujengaka na utamaduni wa kusaidia kuleta maendeleo ya watu wenye ulemavu.
                                       
                      MAADILI YA M.C.F
Kuwa muadilifu, kuonesha huruma na upendo kwa watu wenye mahitaji maalumu,kusema kweli.
                                   
                       MALENGO YA M.C.F
1.Kutafuta misaada ya mbalimbali ya kijamii kwaajili ya kuziwezesha familia zinazo ishi na watoto wenye ulemavu pamoja na mayatima.
2.Kukuza ustawi wa makundi maalumu ya watu wenye ulemavu
3.Kuelimisha jamii kuhusiana na sheria za taiifa na kimataifa zinazofungamana na watu wenye ulemavu. 

No comments:

Post a Comment